Uchanganuzi wa Majina ya Wanaume Katika Jamii ya Watugen

https://doi.org/10.51317/eajk.v5i1.887

Authors

Keywords:

Jamii na simiotiki, maana ya majina, majina ya wanaume, sherehe za kupeana majina

Abstract

Swahili

Utafiti huu ulichambua majina ya wanaume katika jamii ya Watugen, Kaunti ya Baringo ya Kati, Kenya. Lengo kuu lilikuwa kuchunguza majina haya miongoni mwa wanajamii wa eneo hilo. Ingawa majina ya kipekee katika jamii hii hujumuisha yale yanayotokana na mito, milima, vijiji, miji, watu na nchi, uchunguzi ulijikita kwenye majina ya wanaume pekee. Makala hii inajumuisha vijisehemu vifuatavyo: maelezo mafupi kuhusu jamii ya Watugen, utamaduni wa kupeana majina, sherehe zinazohusiana na kupeana majina, majina ya wanaume pamoja na maana zao, na hitimisho. Utafiti uliongozwa na nadharia ya simiotiki, ambayo inasisitiza kuwa kila ishara ina maana yake maalum. Data zilikusanywa kwa njia ya uchunguzi wa nyanjani kwa kutumia mbinu ya mahojiano. Washiriki 50, ambao walikuwa watu wazima wenye umri kati ya miaka 35 na 70, walihojiwa kwa muda wa majuma mawili. Sampuli ya majina iliorodheshwa katika majedwali ili kuwezesha uchambuzi. Utafiti uliongozwa na maswali yanayohusu Watugen ni watu wa wapi, sherehe zipi zilihusiana na kupeana majina, sababu za ujinaishaji zilikuwa zipi, kategoria zipi za majina zilikuwepo, na maana za majina ya wanaume zilikuwa zipi. Majibu ya maswali haya yaliunda kiini cha utafiti. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa majina ya wanaume yalitokana na hali halisi za kijamii katika jamii ya Watugen, na kila jina likibeba maana maalum. Ilibainika kuwa ujio wa wageni, hasa wamishonari, uliathiri sana mchakato wa ujinaishaji. Zaidi ya hayo, majina hayo yana miundo mbalimbali

English

This study analysed male names in the Tugen community, Central Baringo County, Kenya. This study aimed to analyse male names among members of the Watugen community in Central Baringo County, Kenya, East Africa. Although proper nouns include names of rivers, mountains, villages, towns, people, and countries, this study covered only male names. This article comprises the following sections: a brief description of the Tugen community; naming culture; naming ceremonies; male names and their meanings; and conclusions. This study was guided by semiotic theory. Semiotic theory holds that each sign has its own specific meaning. Data collection was conducted in the field. An interview method was used to collect data from 50 adults aged 35-70 over two weeks. A sample of names was listed in tables. The following questions guided this study: Where are the Tugen people? What ceremonies were associated with naming? What were the reasons for naming? What categories were there? What were the meanings of male names? The answers to these questions are the focus of this study. The study found that male names reflected the realities of the Tugen community, and each name carried a unique meaning. It was also found that the arrival of foreigners, mostly missionaries, affected the naming process in the Tugen community. In addition, it was established that these names have various structures.


Keywords: Male names, meaning of names, naming ceremonies, society and semiotic.

 

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2026-03-18

How to Cite

Bowen, D. (2026). Uchanganuzi wa Majina ya Wanaume Katika Jamii ya Watugen. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 5(1), 24–31. https://doi.org/10.51317/eajk.v5i1.887

Issue

Section

Articles

Similar Articles

<< < 1 2 

You may also start an advanced similarity search for this article.