Matumizi ya Umajazi wa Kitashtiti katika Usawiri wa Wahusika na Maudhui katika Riwaya: Mfano wa Riwaya ya Tumaini

https://doi.org/10.51317/eajk.v3i1.471

Authors

Keywords:

maudhui, riwaya, tashtiti, umajazi, umuundo, wahusika

Abstract

SWAHILI

Makala hii iliazimia kuhakiki matumizi ya mbinu ya umajazi wa kitashtiti katika kukuza wahusika na kuendeleza maudhui katika riwaya ya Tumaini ya Clara Momanyi. Madhumuni ya karatasi hii ni kuchanganua namna mbinu ya umajazi wa kitashtiti umetumiwa kuwakuza wahusika na kuendeleza maudhui katika riwaya ya Tumaini. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Umuundo. Wataalamu kama Scholes (1974) na Olsen (1973) wanashikilia mawazo kwamba ni muhimu kutumia Umuundo katika uhakiki wa maandishi ya fasihi kwa sababu lugha na fasihi zina uhusiano mkubwa sana. Matumizi ya Umuundo katika uhakiki wa fasihi hutuelekeza kuitazama fasihi kama mfumo ambao unajumlisha vipengele kama: Fani na maudhui ambavyo huchangia ukamilifu wake. Vipengele hivi huchangiana na kukamilishana katika kazi ya fasihi kama vile riwaya. Nadharia hii ya Umuundo ilitusaidia kuhakiki namna mbinu ya umajazi wa kitashtiti umetumiwa kusawiri wahusika na kuendeleza maudhui katika riwaya ya Tumaini. Ukusanyaji wa data ulifanyika maktabani. Riwaya teule na makala zinazohusiana na mada zilisomwa. Data zilidondolewa, zilichujwa, zilichunguzwa na kisha zilichanganuliwa kwa kutumia majedwali na asilimia ya majina ya majazi ya kitashtiti. Data zilizokusanywa pia zilitumiwa kuhakiki matumizi ya umajazi wa kitashtiti katika kuwakuza wahusika na kuendeleza maudhui katika riwaya ya Tumaini. Pia, tuligundua kwamba mbinu ya matumizi ya umajazi wa kitashtiti yana mchango mkubwa kuwasawiri wahusika na kuyaendeleza maudhui katika riwaya ya Tumaini. Aidha, matokeo ya utafiti huu yatasaidia wahakiki, waandishi, walimu na wanafunzi wa shule za upili na hata vyuoni kuhakiki matumizi ya majina ya kimajazi katika kazi za fasihi andishi. Mbali na kazi hii kuwafaidi wahakiki, matokeo ya utafiti huu yatakuwa na mchango mkubwa katika kuwahamasisha waandishi chipukizi kutumia mbinu ya umajazi wa kitashtiti katika harakati zao za utungaji riwaya.

ENGLISH

This article aimed to examine the use of satirical naming (umajazi wa kitashtiti) in developing characters and advancing themes in Clara Momanyi's novel Tumaini. The purpose of this paper is to analyze how the technique of satirical naming has been employed to construct characters and develop themes in the novel Tumaini. The study was guided by Structuralist theory. Scholars such as Scholes (1974) and Olsen (1973) argue that it is essential to apply Structuralism in the analysis of literary texts because language and literature are closely interconnected. The application of Structuralism in literary criticism directs us to view literature as a system that integrates elements such as form (fani) and content (maudhui), which together contribute to its completeness. These elements interact and complement one another in a literary work, such as a novel. This Structuralist approach helped us evaluate how the technique of satirical naming was used to portray characters and develop themes in Tumaini. Data collection was conducted through library research. The selected novel and related articles on the topic were read. Data were extracted, filtered, examined, and then analyzed using tables and percentages of satirical names. The collected data were also used to assess the application of satirical naming in character development and theme advancement in Tumaini. Furthermore, we discovered that the technique of satirical naming makes a significant contribution to portraying characters and advancing themes in the novel Tumaini. In addition, the findings of this study will benefit literary critics, writers, teachers, and students in secondary schools and even universities in analysing the use of symbolic or allegorical names in written literary works. Beyond aiding critics, the results of this research will make a substantial contribution to encouraging emerging writers to employ the technique of satirical naming in their novel-writing endeavors.

Keywords: Themes, Novel, Satire, Onomastic Device, Structuralism, Characters.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2024-02-08

How to Cite

Bowen, D. (2024). Matumizi ya Umajazi wa Kitashtiti katika Usawiri wa Wahusika na Maudhui katika Riwaya: Mfano wa Riwaya ya Tumaini. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 3(1), 1–7. https://doi.org/10.51317/eajk.v3i1.471

Issue

Section

Articles

Similar Articles

1 2 > >> 

You may also start an advanced similarity search for this article.